Thursday, November 11, 2010
SAFARI YA KUWASILI MJENGONI HIYOOO.........
Wa Kwanza Kushoto ni Ezekiel Dibogo Wenje, mbunge mteule kwa tiketi ya CHADEMA katika jimbo la Nyamagana Mwanza....wa katikati (nyuma) ni Hyness Kiwia, mbunge mteule kwa tiketi ya CHADEMA katika jimbo la Ilemela Mwanza na wa kulia ni Felix Mkosamali (Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu SAUT) ambaye ni Mbunge mdogo kuliko wote (Miaka 24) toka NCCR Mageuzi katika jimbo la Muhambwe Kigoma.
Baadhi ya Wabunge wateule wakiwa wanasalimiana na aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Mheshimiwa Samuel Sitta (wa Pili kutoka kulia).
Aliyekuwa kiongozi wa Kambi ya Upinzani Mheshimiwa Hamad Rashid (kushoto) akisalimiana na aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samuel Sitta. Wote wamezikosa nafasi hizo za awali katika Bunge la Kumi.
Mbunge mteule wa jimbo la Same Mashariki Kilimanjaro (CCM) Mheshimiwa Anne Kilango-Malecela akimpokea kwa furaha Mbunge mteule wa jimbo la Hai Kilimanjaro (CHADEMA) Mheshimiwa Freeman Mbowe.
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Dokta Wilbroad Slaa akiwasili katika viwanja vya Bunge kwa ajili ya Mkutano wa ndani wa chama hicho kati ya viongozi na Wabunge wateule wa CHADEMA.
Moja kati ya Wabunge wateule waliowasili na kufurahiwa basi ni Mheshimiwa Agustino Lyatonga Mrema wa Vunjo Kilimanjaro. Hapo alikuwa akipokewa na Mheshimiwa Sitta. Ni kama wengi hawaamini kumuona kwa mara nyingine tena mjengoni.
Kila la kheri kwa wote waliochaguliwa kwa ridhaa ya Wananchi. Zoezi la usajili kwa Wabunge hao limekwishahitimishwa. Kuanzia Jumamosi hii wataanza kula viapo vyao kabla ya kuwa Wabunge rasmi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment