Wednesday, March 31, 2010

UFUNDI WA KUPIGA PICHA

Wahenga wanasema ukistaajabu ya Musa basi jiandae kuyashuhudia ya Filauni. Habari za sasa hivi Mabibi na Mabwana. Kwanza nikushukuru wewe ambaye umeamua kuwa mfuasi wa kutaka kujua kilichomo ndani ya ukurasa huu.

Sasa kuna kitu kinaitwa UPIGAJI PICHA. Ni katika Picha hizi hizi tunazozihifadhi kwa ajili ya kumbukumbu zetu mbalimbali. Ama kweli usione tu Picha imetoka na ukaifurahia kweli. Ebu jaribu kuwaangalia Wapiga Picha huwa wanakuwaje, wamekaaje ama wamesimamaje wakati wanapiga Picha hizo?



Nakumbuka Mwalimu wangu katika fani ya upigaji Picha pale SAUT anaitwa Barack Omollo Othyeno aliniambia kuwa ‘mbwembwe’ za Picha ama uzuri wa Picha unategemea na Mpiga Picha alikuwa amejiweka wapi wakati anapiga Picha husika (POSITIONING). Ukijiweka vibaya ama vizuri wakati unaiwinda Picha yako, basi Picha hiyo itakuwa kadiri ulivyojiweka wewe mwenyewe.



Katika pitapita zangu hususani katika matukio mbalimbali ambayo nimekuwa nahudhuria, basi Kamera yangu imekuwa inawaangalia Wapiga Picha na Mapozi yao. Na haya ndio niliyoyaona!

























HAPO VIPI??????????????????????