Wednesday, November 24, 2010

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI 2010 - 2015

MUHIMU:
 Wizara ya Maji imeunganishwa na Kilimo na hivyo itakuwa ni Wizara ya Kilimo na umwagiliaji. Hapa Kilimo kwanza kimeongezewa nguvu ili kuondokana na kilimo cha msimu.
 Kazi, ajira na Vijan; kitengo cha Vijana kimehamishiwa Michezo na Utamaduni.
 Uwezeshaji wa Wananchi (Baraza la Uwezeshaji) ilikuwa katika Wizara ya Fedha na sasa imebidi kuipunguzia Hazina mzigo huu na kuielekeza Ofisi ya Waziri Mkuu.
 Wizara ya Miundombinu imepunguzwa, imegawanywa na kuwa na Wizara ya Ujenzi (Barabara na Viwanja vya Ndege) pamoja na Wizara ya Uchukuzi (Reli, Bandari na Usafiri wa Majini).


BARAZA LA JIPYA LA MAWAZIRI Lililotangazwa November 24, 2010
1. Waziri wa nchi Ofisi ya Rais; Uhusino na Uratibu – Stepehn Wasira
2. Waziri wa nchi ofisi ya rais; Menejiment ya Utumisi wa umma – Hawa Ghasia
3. Waziri wa nchi makamu wa Rais; Muungano - Samia Suluhu Hassan
4. Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu; Mazingira - Therezia Luoga Kofisa
5. OWM; Sera Uratibu na bunge – William Lukuvi
6. OWM; Uwekezaji na Uwezeshaji – Maria Nagu
7. OWM; TAMISEMI - George Mkuchika
8. OWM; Naibu Waziri TAMISEMI – Agrey Mwanri
9. OWM; Naibu Waziri – Elimu – Khassim Majali
10. Waziri wa Fedha – Mustafa Mkulo
11. Naibu waziri wa Fedha – Gregory Teu
12. Naibu Waziri Fedha – Bereila Ame Silima
13. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi – Shamsi Vuai Nahodha
14. Naibu Waziri Mambo ya Ndani – Khamis Kagasheki
15. Waziri wa Katiba na Sheria – Celina Kombani
16. Waziri Mambo ya nje – Bernad Membe
17. Naibu Waziri Mambo ya Nje – Mahadhi Juma Mahadi
18. Waziri wa ulinzi na JKT – Dk. Hussein Ally Hassan Mwinyi
19. Waziri wa Mendeleo ya Mifugo- Mathayo David mathayo
20. Naibu waziri Maendeleo ya Mifugo – Benedict Ole Nangolo
21. Wizari ya Mawasilaino Sayansi, Tekonolojia, – Prof. Makame Mnyaa Mbalawa
22. Naibu Waziri Mawasilaino Sayansi, Teknolojia – Charles Kiwanga
23. Waziri Ardhi Nyumba na makazi – Prof Anna Tibaijuka
24. Naibu Waziri Ardhi Nyumba na makazi – Godluck Ole Medeye
25. Waziri wa mali Asili an Utalii – Ezeki el Maige
26. Waziri wa Nishati na Madini – William Ngeleja
27. Naibu waziri wa Nishati na Madini - Adam Malima
28. Waziri Ujenzi wa Barabara, Viwanja vya Ndege – John Pombe Mgufuli
29. Naibu Waziri wa Barabara, Viwanja vya Ndege – Harrison Mwakyembe
30. Waziri wa Uchukuzi – Bandari, Reli, Majini – Omary Nongwi
31. Naibu waziri Bandari, Reli, Majini – Athuman Mfutakamba
32. Waziri wa Viwanda na Biashara – Cyril Chami
33. Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara- Lazaro Nyalandu
34. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi – Shukuru Kawambwa
35. Naibu Waziri Elimu na Mafunzo ya Ufundi- Philipo Murugo
36. Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii – Hussein Haji Mpanda
37. Naibu waziri Afya na Ustawi wa jamii – Lucy Nkya
38. Waziri wa Kazi na Ajira – Gaudencia Kabaka
39. Naibu waziri kazi na Ajira -Makongoro Mahanga
40. Waziri maendeleo ya jamii Jinsia na Watoto – Sophia Simba
41. Naibu Waziri Ummy Ally Mwalimu
42. Waziri wa Elimu, Habari, vijana na Michezo – John Nchimbi
43. Naibu Waziri Elimu, Habari, vijana na Michezo – Fenela Mkangala
44. Waziri wa ushirikiano Afrika mashariki – Samuel Sitta
45. Naibu Waziri Dk Abdalah Juma Abdalah
46. Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika – Jumanne Maghembe
47. Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika – Christopher Chiza
48. Waziri wa maji – Mark Mwandosya
49. Naibu Waziri wa maji – Gerson Luende
50. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais; Utawala Bora - Mathias Chikawe

Thursday, November 11, 2010

KINYANG'ANYIRO CHA USPIKA CCM.....

Viwanja vya Bunge mjini Dodoma vimetawaliwa na Vazi la Kijani leo baada ya zaidi ya Wabunge 200 wa Chama cha Mapinduzi CCM kukusanyika pamoja kwa ajili ya uchaguzi wa Mgombea wa Uspika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Siku ya Alhamisi Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi ilikutana katika Makao Makuu ya Chama hicho na kuyachuja Majina ya Wagombea 15 waliokuwa wameomba ridhaa hiyo. Jukumu la Kamati hiyo lilikuwa ni kubakiza Majina Matatu tu na ndipo:

Mama ANNA MAKINDA.....

Mama Makinda akiomba kura kutoka kwa Mmoja wa wajumbe wa Mkutano wa Kamati ya Wabunge wa CCM.

Mama ANNA ABDALAH.....

Hapo Mama Abdalah mwenye Kijani akiomba kura kutoka kwa Mama Sophia Simba muda mfupi kabla kuanza kwa uchaguzi.

Na Mama KATE KAMBA....

Mama Kamba akiomba kura kutoka kwa Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda kabla ya kufanyika kwa uchaguzi.

Basi hao ndio Wagombea Watatu waliopita katika mchujo huo wa NEC. Wote watatu ni Wanawake. Kwa nini?

Katibu wa CCM Yusuf Makamba anasema kuwa ni mpango wa makusudi wa chama chao ukilenga kuchochea zaidi vuguvugu la harakati za kumkomboa Mwanamke. Wanaamini kwa kufanya hivyo, mgombea atakayepita basi atakiwakilisha chama vizuri katika kinyang'anyiro cha Uspika na hatimaye Bunge hilo kupata kiongozi wake mkuu ambaye ni Mwanamke.

Tangu Tanzania imepata uhuru haijawahi kuwa na kiongozi mkuu mwanamke katika mihili yake yote mitatu ya nchi. Na Makamba anasema wamedhamiria kuifuta rekodi hiyo nchini na hatimaye kuandika historia mpya kwa moja ya mihili mitatu ya Taifa kuongozwa na Mwanamke. Ni mpango mzuri kwa kweli unaolenga kumkweza Mwanamke MWENYE UWEZO WA KUONGOZA. Mpango huo utawezekana? Tusubiri tuone.

Rungu la Kamati ya Wabunge wa CCM limekaa pia na kupiga kura za maoni za kumchagua mgombea mmoja kati ya hao Watatu. Na baada ya uchaguzi huo, taarifa iliyotolewa na Katibu Mwenezi wa CCM Kepteni John Chiligati ni kuwa Mheshimiwa ANNA MAKINDA ndiye mgombea wa uspika wa Bunge la Kumi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



Mama Makinda amepata kura 211 kati ya 241 zilizopigwa. Mama Abdalah amepata kura 14 wakati Mama Kamba amepata kura 15, huku kura Moja tu ikiharibika.

Je, enzi za 'zama za spidi na viwango ndio zimeisha?'


"...amani ya ndani ya Bunge ni kanuni...," ni kati ya kauli alizozitoa Mama Makinda kuhusiana na utendaji wake wa kazi bungeni endapo atapata nafasi ya kuiongoza taasisi hiyo. Anasema kila jambo lina taratibu zake na hivyo kila Mbunge anapaswa kuzielewa kwa umakini kanuni zinazoliongoza Bunge ili awe na mahusiano mazuri na kiti cha Spika na akimalizia, "....ni kama mpira wa Miguu, lazima ucheze kwa kufuata sheria...."



Furaha kama hiyo itadumu endapo Mama Makinda atashinda uchaguzi wa Spika. Katika kinyang'anyiro hicho anakumbana na Wakili MABERE MARANDO ambaye amepitishwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA. Wabunge kwa umoja wao wataamua wanamuhitaji nani kati ya hao Wawili ili awe Spika wao mpya.

Ikumbukwe kuwa, hili ni Bunge lililotokana na hamasa ya Siasa waliyonayo Watanzania kwa hivi sasa. Ni hamasa hiyo iliyopelekea Bunge la Kumi kuongeza Wabunge wa kambi ya Upinzani....kuongeza kundi la Vijana kutoka Vyama vyote....kuongeza kundi la Wasomi......na hata viongozi wa dini.

Spika ajae ni vyema akaliangalia ongezeko la makundi hayo na kujua namna ya kufanya nayo kazi kwa pamoja bila mikwaruzano ya hapa na pale hisiyo na msingi kwa maendeleo ya Mtanzania.

Kila la kheri Mama Anna Makinda.....

MWANZO MZURI WA UGENINI.....

Baada ya kuona hizi Picha zifuatazo nikapata fikra kuwa kumbe mwanzo mzuri wa kuwa ugenini ni pale unapopata mapokezi mazuri kutoka kwa wenyeji wako:


Mheshimiwa Freeman Mbowe akikaribishwa mjengoni na Mheshimiwa Anna Kirango.


Mheshimiwa Samwel Sitta akimkaribiwa mjengoni Mheshimiwa Lyatonga Mrema.

SAFARI YA KUWASILI MJENGONI HIYOOO.........



Wa Kwanza Kushoto ni Ezekiel Dibogo Wenje, mbunge mteule kwa tiketi ya CHADEMA katika jimbo la Nyamagana Mwanza....wa katikati (nyuma) ni Hyness Kiwia, mbunge mteule kwa tiketi ya CHADEMA katika jimbo la Ilemela Mwanza na wa kulia ni Felix Mkosamali (Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu SAUT) ambaye ni Mbunge mdogo kuliko wote (Miaka 24) toka NCCR Mageuzi katika jimbo la Muhambwe Kigoma.


Baadhi ya Wabunge wateule wakiwa wanasalimiana na aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa Mheshimiwa Samuel Sitta (wa Pili kutoka kulia).


Aliyekuwa kiongozi wa Kambi ya Upinzani Mheshimiwa Hamad Rashid (kushoto) akisalimiana na aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samuel Sitta. Wote wamezikosa nafasi hizo za awali katika Bunge la Kumi.


Mbunge mteule wa jimbo la Same Mashariki Kilimanjaro (CCM) Mheshimiwa Anne Kilango-Malecela akimpokea kwa furaha Mbunge mteule wa jimbo la Hai Kilimanjaro (CHADEMA) Mheshimiwa Freeman Mbowe.


Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Dokta Wilbroad Slaa akiwasili katika viwanja vya Bunge kwa ajili ya Mkutano wa ndani wa chama hicho kati ya viongozi na Wabunge wateule wa CHADEMA.


Moja kati ya Wabunge wateule waliowasili na kufurahiwa basi ni Mheshimiwa Agustino Lyatonga Mrema wa Vunjo Kilimanjaro. Hapo alikuwa akipokewa na Mheshimiwa Sitta. Ni kama wengi hawaamini kumuona kwa mara nyingine tena mjengoni.


Kila la kheri kwa wote waliochaguliwa kwa ridhaa ya Wananchi. Zoezi la usajili kwa Wabunge hao limekwishahitimishwa. Kuanzia Jumamosi hii wataanza kula viapo vyao kabla ya kuwa Wabunge rasmi.

Wednesday, November 10, 2010

KIVUMBI IDODOMYA


Ziliaanza Kampeni na hatimaye Uchaguzi Mkuu umefanyika....viongozi nao wamepatikana: Madiwani, Wabunge na Rais. Mhiumili wa Tatu wa Nchi ni Bunge ambalo nalo pia lina Uongozi wake chini ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Spika Samuel Sitta (Mwenye Suti ya Kijivu akisalimiana na Wageni wa Bunge) ndiye alikuwa Kiongozi wa Taasisi hiyo katika Bunge la Tisa....na sasa ni Bunge la Kumi lenye ongezeko la Vijana....ongezeko la Wapinzani pia.


Mmoja wa Maafisa wa Bunge akiwa amebeba na kuyaingiza bungeni Majoho ya Spika na Naibu wake. Ni nani atachukua dhamana ya kuliongoza Bunge hilo? Chama cha Mapinduzi CCM kimepata Wagombea Kumi na Tatu; Chaama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimepata Wagombea Watano.

CCM wameshafanya mchujo na kuwabakiza Watatu: ANNA ABDALAH, ANNA MAKINDA na KATE KAMBA; CHADEMA kupitia kwa Mwenyekiti wao Freeman Mbowe hawakuweka hadharani ni nani wamempendekeza kuwania nafasi hiyo lakini tayari taarifa za kuaminika kutoka ndani ya chama hicho zinasema kuwa ameteuliwa MABERE MARANDO. Vita ni Vita Muraa!!!!

Tuvute subira kwani uchaguzi ni Ijumaa.