Monday, August 23, 2010

J. K. NDANI YA MWANZA

Kipenga cha Kampeni za Wagombea wa nafasi za Urais, Ubunge na Udiwani katika mwaka huu wa uchagazi, ndivyo hivyo kimeshapulizwa. Chama tawala...Chama cha Mapinduzi CCM kupitia kwa Mgombea wake urais Jakaya Kikwete na mgombea mwenza wake Ghalib Bilal imeshazindua rasmi kampeni zake huko jijini Dar es Salaam.

Baada ya Dar es Salaam, mambo yakaamia jijini Mwanza katika wilaya za Misungwi, Kwimba, Nyamagana na hatimaye uwanja maarufu wa CCM Kirumba.

Watu wakajitokeza kwa wingi kuwashuhudia Wagombea hao wa CCM:


Msafara ukaongozwa na Vijana waendesha pikipiki ambao hapa kwa Mwanza wanajulikana kwa jina maarufu la BODABODA kutokana na huduma wanayoitoa ya kubeba abiria:


Wanafunzi nao walijitokeza kama wanavyoonekana hapo wakiwa wamejipanga kumlaki mgombea urais wa CCM na timu yake:


Vijana wa CCM nao wakajipanga vilivyo kufanikisha tukio la Kampeni za CCM ndani ya jiji la Mwanza katika dimba la CCM Kirumba:






Na kisha Wagombea Urais na Umakamu wa rais wa CCM wakaonekana:




Hatimaye Wagombea hao wakajinadi kwa Wananchi wa Mwanza, wakisifu jitihada mbalimbali ambazo zimefanywa na Serikali ya awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake Ali Shein. Maeneo yaliyotajwa ni pamoja na Michezo, Miundombinu, Elimu, Afya na huduma za nishati na Maji vijijini.

Maeneo waliyoahidi kuyafanyia kazi zaidi ni kuboresha miundombinu ya Safari za Vivuko, Mwanza - Sengerema kupitia Kamanga; Ujenzi wa Nyumba za Walimu kwa kutumia pesa za ndani badala ya kuwategemea Wafadhili, kuiongezea Pesa benki ya rasilimali ili iweze kutoa mikopo zaidi kwa Wanawake na Vijana waweze kujiajili.

Hayo ni machache kati ya mengi tu ambayo CCM imekusudia kuyafanya kupitia ilani yake ya uchaguzi ya Mwaka 2010. Kiu ni utekelezaji wa hayo yanayohubiriwa na wanasiasa kwani katika kipindi hiki sauti za Wanasiasa zitahubiri mengi tu.

Ni wajibu wako Mwananchi kuyasikiliza....kuyatafakari na kuona kama yanatekelezeka.....lakini cha muhimu zaidi ni kwa wewe kutothubutu hata chembe kupuuzia kushiriki katika zoezi la kupiga kura. Maamuzi yako ni muhimu sana kwa ustawi bora wa nchi hii.

Mungu ibariki Tanzania. Mungu ubariki uchaguzi wa 2010.

Friday, August 13, 2010

FOLENI NDANI YA MWANZA

Mipango Miji bado inatupiga chenga sana. Mimi nilidhani Wahandisi wetu wa Miji inayokuwa kwa kasi hapa nchini wanatakuwa wanajifunza kwa uzoefu wa jiji la Dar es Salaam jinsi linavyopata shida ya foleni!!!

Lakini ni tofauti kwani sikutarajia kuona jiji la Mwanza linaanza kuona shubiri ya foleni ikiwa bado ni mapema sana. Watendaji wa jiji hawakushtuka toka mapema? Matokeo yake mambo haya kwa Mwanza yameshaanza kuzoeleka sasa wakati ndiyo kwanza jiji linaanza kukua kwa kasi.

Poleni Mwanza. Tumeshachelewa. Sasa hivi mjini kutakuwa hakuendeki.

TUSEME NI USAFIRI KAFIRI AU!!!??

Hivi karibuni tu tumesikia huko wilayani Sengerema Wanafunzi wakizama na kupoteza maisha. Mkasa wenyewe ni kutokana na usafiri wa Mtumbwi waliokuwa wakiutumia kwenda shule kuingiwa maji na kisha kushindwa kuhimili uzito wa maji na abiria walokuwemo na matokeo yake Mtumbwi wa Mv School Boat kuzama, mwisho wa siku Wanafunzi 19 wakapoteza maisha.


Lakini maisha ya Watu wa visiwani ndivyo yalivyo kila siku. Usafiri wao ni wa Mitumbwi tu iwe ni kutoka visiwani ama kurudi visiwani. Hawana vifaa vya kujikinga na maafa pindi wanapokuwa safarini. Hawana hata vifaa vya kujiokoa pindi ajali inapotokea na ndiyo hata maana wakati wa msiba wa Wanafunzi hao, ni Nyavu haramu aina ya Makokoro zinazokatazwa kwenye uvuvi lakini ndizo zilizokuwa mwokozi wa kufanikisha zoezi la kuopoa Maiti za Wanafunzi. Kwa faida yako tu ni kuwa Makokoro ndiyo yaliyotumika kuzonasa Maiti mithili ya Samaki wanavuliwa!!!!!!

Licha ya ajali kama hizo kuwa zinatokea mara kwa mara lakini hakuna mabadiliko katika usalama wa safari kama hizo za kwenda katika visiwa vidogovidogo. Ukizama ni ujanja wako tu wa kupiga mbizi. Si unaona kama hao jamaa chini hapo wanapiga Safari katika maeneo yenye kina kirefu halafu hawana tahadhali yoyote!!!!

Lakini ukweli unabaki pale pale kuwa ajali ni ajali tu. Hata Nyani hufa tu siku Miti yote anayoirukia akitereza. Ila kwa nini tahadhali ziwepo jamani!!!!!?????