Hivi karibuni tu tumesikia huko wilayani Sengerema Wanafunzi wakizama na kupoteza maisha. Mkasa wenyewe ni kutokana na usafiri wa Mtumbwi waliokuwa wakiutumia kwenda shule kuingiwa maji na kisha kushindwa kuhimili uzito wa maji na abiria walokuwemo na matokeo yake Mtumbwi wa Mv School Boat kuzama, mwisho wa siku Wanafunzi 19 wakapoteza maisha.
Lakini maisha ya Watu wa visiwani ndivyo yalivyo kila siku. Usafiri wao ni wa Mitumbwi tu iwe ni kutoka visiwani ama kurudi visiwani. Hawana vifaa vya kujikinga na maafa pindi wanapokuwa safarini. Hawana hata vifaa vya kujiokoa pindi ajali inapotokea na ndiyo hata maana wakati wa msiba wa Wanafunzi hao, ni Nyavu haramu aina ya Makokoro zinazokatazwa kwenye uvuvi lakini ndizo zilizokuwa mwokozi wa kufanikisha zoezi la kuopoa Maiti za Wanafunzi. Kwa faida yako tu ni kuwa Makokoro ndiyo yaliyotumika kuzonasa Maiti mithili ya Samaki wanavuliwa!!!!!!
Licha ya ajali kama hizo kuwa zinatokea mara kwa mara lakini hakuna mabadiliko katika usalama wa safari kama hizo za kwenda katika visiwa vidogovidogo. Ukizama ni ujanja wako tu wa kupiga mbizi. Si unaona kama hao jamaa chini hapo wanapiga Safari katika maeneo yenye kina kirefu halafu hawana tahadhali yoyote!!!!
Lakini ukweli unabaki pale pale kuwa ajali ni ajali tu. Hata Nyani hufa tu siku Miti yote anayoirukia akitereza. Ila kwa nini tahadhali ziwepo jamani!!!!!?????
No comments:
Post a Comment