Saturday, January 30, 2010

MJENGO HUO WA DUNIA


Hilo ndilo jengo lenyewe....refu kuliko yote katika Dunia hii. Kabla ya Dunia kulishuhudia tukio hilo la kihistoria, mkuu wa Dubai Sheikh Mohammad bin Rashed al-Maktoum aliondoa kitambaa kilichofunika mnara wa jengo hilo, akiashiria kuwaaaaa limefunguliwa rasmi, na ndipo Dunia ikashuhudia live historia hiyo.

Huo Mjengo ni mjengo wa Burj Khalifa uliopo huko Dubai....mjengo unaosifiwa kuwa ni mjengo mrefu zaidi duniani.

Ebu ona linavyopasua anga na kuleta mandhari nzuuuri kweli kweli. Ni mambo ya Dunia hayo.


Jina la mjengo huo yaani Burj Khalifa limenatokana na jina la rais Khalifa Bin Zayed Al-Nahyan wa Umoja wa Falme za Kiarabu ambaye pia ni mkuu wa Abu Dhabi. Na Tarehe 4 yaani siku lilipozinduliwa jengo hilo ni siku ambayo ilitimia miaka minne tangu mkuu wa Dubai Sheikh Mohammad bin Rashed al-Maktoum aingie madarakani.

Jengo la Burj Khalifa lenye urefu wa mita 828 ni jengo refu zaidi duniani, ambalo limesifiwa kuwa ni mji uliosimama wima. Na kwenye jengo hilo lenye ghorofa 160, kuna nyumba, ofisi na hoteli za anasa. Inakadiriwa kuwa watu elfu 12 wanaweza kuishi kwenye jengo hilo.

Siku ya ufunguzi Watu kibao walienda karibu na jengo hilo ili kushuhudia kwa Macho yao wenyeeeewee. Wengine Mamilion walishuhudia kupitia Runinga zao kote Duniani.


Haya, ni vijimambo tu vya kuashiria kuwa Dunia inazidi kubadilika.