Monday, December 14, 2009

USAFIRI WA PIKIPIKI

Mwaka huu Bunge letu la Jamhuri ya muungano wa Tanzania liliifanyia marekebisho Sheria ya Usafirishaji na hatimaye Pikipiki na Baiskeli zimeruhusiwa kupakia Abiria kibiashara kwa kutoza Nauli.

Lakini kwa upande wa Pikipiki, utaratibu huu una masharti yake. Dereva wa Pikipiki anatakiwa kuzifahamu sheria za barabarani ikiwemo na kuwa na leseni. Dereva na Abiria wa Pikipiki wanatakiwa kuvaa Kofia maalumu kichwani a.k.a HELMET.

Aina hii ya usafiri wa abiria kwa kutumia Pikipiki a.k.a BODABODA kwa baadhi ya maeneo kama unavyojulikana hususani kanda ya ziwa, umeanza kuwa maarufu sana kwa sababu ni wa haraka na isitoshe bei ni nafuu ukilinganisha na usafiri mwingine wa haraka mathalani Taksi.
Tatizo sasa ni kutokufuatwa kwa sheria za barabarani huku Madereva wengi wao wakiwa ni vijana kusemekana kuwa wanaendesha hovyo huku utafiti wa kipolisi ukisema kuwa wengi wao huwa wanaingia barabarani wakiwa wamefyonza viroba!

Cha ajabu kingine ni kwamba si jambo la ajabu sana kukuta aidha Dereva amevaa HELMET huku abiria akiwa hana au kibaya zaidi kukuta wote (Dereva na Abiria) hawana hiyo HELMET.

Mpya kuliko zote sasa. Kuna tabia ya kupakia Abiria zaidi ya mmoja. Unakuta Dereva wa Pikipiki kapakia Abiria Wawili au zaidi katika Pikipiki moja! Mtindo huo wa upakiaji kwa huku Mwanza unajulikana kama MSHIKAKI!
Lakini hata sheria hiyo iliyobarikiwa na Bunge inasisitiza matumizi sahihi ya Pikipiki likiwemo hilo la kupakia Abiria mmoja tu katika Pikipiki.
Hawa Madereva ni viburi kwa kisingiziio kuwa Bunge limeubariki usafiri huo. Inastaajabisha kuwa Pikipiki hiyo iliyopakia Abiria zaidi ya mmoja inakatiza mbele ya Macho ya Askari wa barabarani na wala hakuna hatua zinazochukuliwa.
Kutokana na uzembe huo pamoja na mengine niliyoyataja hapo juu ndani ya usafiri huu wa Pikipiki, baadhi ya mikoa imeshuhudia kuongezeka kwa ajali za usafiri wa Pikipiki. Watu wanakufa. Watu wanapata majeraha ya kudumu.
Mikoa mingine katika hospitali zao za mikoa na nyingine za rufaa imefikia hatua ya kutenga wodi maalumu za majeruhi wa pikipiki!
Tunakwenda wapi? Tunawafanya nini hawa Madereva Pikipipiki. Tunaudhibiti usafiri huu ili usiendelee kugharimu maisha ya Watanzania?

KAZI YETU YA UANDISHI WA HABARI

UCHUKUAJI PICHA NA STYLE ZAKE




MAHOJIANO NA KUCHUKUA DONDOO MUHIMU



MAENEO MENGINE KAMA YA IRAQ NA KWINGINEKO KWENYE SHURBA, UKAGUZI KWANZA KAZI BAADAE


WENGINE UBABE UKIWAZIDI KINACHOTOKEA NI WAANDISHI KUPIGWA NA KUHARIBIWA VITENDEA KAZI VYAO




WENGINE HUISHIA KUFUNGWA KISA WAMETIMIZA WAJIBU WAO WA KUTOA HABARI


WANAONUSURIKA HUISHIA KUWATETEA WENZAO, KAMA HAWA WAMEJIFUNGA MIDOMO YAO KUASHIRIA KUWA UHURU WA WAANDISHI WA HABARI NI TATIZO


LAKINI MWISHO WA SIKU JAMII INAPATA HABARI AMBAZO ZIMEWAHENYESHA WAANDISHI HUSIKA KUZIPATA




Lakini hayo yote hayawezi kutukatisha tamaa kwani tumeamua kufanya hii kazi. Tunaielewa. Na isitoshe Jamii inatuhitaji sana kwa kujua kinachooendelea Duniani. Kila mmoja atambue kuwa waandishi ni watu muhimu sana na tunahitaji ushirikiano kwa kazi tunayoifanya.
AMINA.

Thursday, December 10, 2009

BORN WITHOUT LEGS AND ARMS



BORN WITHOUT LEGS AND ARMS

MAITI YAZINDUKA



Kichanga kilisemekana kimekufa! Kikashtuka muda mfupi kabla ya mazishi! Kikafa tena wakati wa matibabu Hospitali.

UHURU BILA MAWAZIRI WAKUU

Eti katika hali hisiyo ya kawaida, Mwaka huu katika maadhimisho ya miaka 48 UHURU wa TZ hakukuwa na Waziri Mkuu wa sasa wala waliostaafu wote!!!!!!!

Hii ni mara ya kwanza kutokea Tz toka tumepata uhuru. Ebu soma Gazeti la Mwananchi unielewe nnachokisema.

Wednesday, December 2, 2009

MWANZA SI MIAMBA TU, BUT ..............PIA.

Jamani eeeeeh? Mwanza is not only the Rock city. Kuna vivutio zaidi ya Mawe vinazidi kumwagika ndani ya Jiji.

Ikawa Usiku, ikawa Asubuhi na haya yakaonekana kweupeeeeeeeeee.

Bofya hapa chini.

Mwanza.