Kipenga cha Kampeni za Wagombea wa nafasi za Urais, Ubunge na Udiwani katika mwaka huu wa uchagazi, ndivyo hivyo kimeshapulizwa. Chama tawala...Chama cha Mapinduzi CCM kupitia kwa Mgombea wake urais Jakaya Kikwete na mgombea mwenza wake Ghalib Bilal imeshazindua rasmi kampeni zake huko jijini Dar es Salaam.
Baada ya Dar es Salaam, mambo yakaamia jijini Mwanza katika wilaya za Misungwi, Kwimba, Nyamagana na hatimaye uwanja maarufu wa CCM Kirumba.
Watu wakajitokeza kwa wingi kuwashuhudia Wagombea hao wa CCM:
Msafara ukaongozwa na Vijana waendesha pikipiki ambao hapa kwa Mwanza wanajulikana kwa jina maarufu la BODABODA kutokana na huduma wanayoitoa ya kubeba abiria:
Wanafunzi nao walijitokeza kama wanavyoonekana hapo wakiwa wamejipanga kumlaki mgombea urais wa CCM na timu yake:
Vijana wa CCM nao wakajipanga vilivyo kufanikisha tukio la Kampeni za CCM ndani ya jiji la Mwanza katika dimba la CCM Kirumba:
Na kisha Wagombea Urais na Umakamu wa rais wa CCM wakaonekana:
Hatimaye Wagombea hao wakajinadi kwa Wananchi wa Mwanza, wakisifu jitihada mbalimbali ambazo zimefanywa na Serikali ya awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake Ali Shein. Maeneo yaliyotajwa ni pamoja na Michezo, Miundombinu, Elimu, Afya na huduma za nishati na Maji vijijini.
Maeneo waliyoahidi kuyafanyia kazi zaidi ni kuboresha miundombinu ya Safari za Vivuko, Mwanza - Sengerema kupitia Kamanga; Ujenzi wa Nyumba za Walimu kwa kutumia pesa za ndani badala ya kuwategemea Wafadhili, kuiongezea Pesa benki ya rasilimali ili iweze kutoa mikopo zaidi kwa Wanawake na Vijana waweze kujiajili.
Hayo ni machache kati ya mengi tu ambayo CCM imekusudia kuyafanya kupitia ilani yake ya uchaguzi ya Mwaka 2010. Kiu ni utekelezaji wa hayo yanayohubiriwa na wanasiasa kwani katika kipindi hiki sauti za Wanasiasa zitahubiri mengi tu.
Ni wajibu wako Mwananchi kuyasikiliza....kuyatafakari na kuona kama yanatekelezeka.....lakini cha muhimu zaidi ni kwa wewe kutothubutu hata chembe kupuuzia kushiriki katika zoezi la kupiga kura. Maamuzi yako ni muhimu sana kwa ustawi bora wa nchi hii.
Mungu ibariki Tanzania. Mungu ubariki uchaguzi wa 2010.
No comments:
Post a Comment