Tusker Project Fame ni shindamo maarufu sana la kuibua vipaji vya Muziki katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati. Kwa Mwaka 2010, shindano hilo ambalo huwa linafanyikia nchini Kenya limefikisha awamu ya Nne huku nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Sudan ya Kusini zikishiriki.
Kwa Mwaka huu 2010, Tanzania iliwakilishwa na mwanadada Aneth Kushaba:
Na kisha akawepo mwanadada mwingine Leah Muddy:
Wadada hao kwa bahati mbaya kura hazikutosha na wakatoka mapema tena kwa kupishana Wiki moja kupitia mtindo maarufu wa mchujo wa ndani ya shindano hilo "PROBATION WEEK."
Mwakilishi wa Tatu kutoka Tanzania akawa ni Peter Mshechu:
Wawakilishi wetu wote wametuwakilisha vizuri tu na wanastahili pongezi. Msechu yeye ameweza kuvuka safari hiyo ndefu ya ushindani na hatimaye akaingia Nusu fainali akiwa na washiriki wenzake Sita kutoka nchi mbalimbali.
Kutoka Kushoto ni Steven (Kenya), Gaelle (Rwanda), Davis (Uganda), Amelina (Kenya), Msechu (Tanzania) na Rachael (Uganda).
Baada ya mchujo huo hatimaye Gaelle na Rachael wakaondoka na Washiriki Wanne waliobaki wakaingia Fainali ambayo imeng'arisha nyota ya Mshiriki Davis wa Uganda aliyeibuka kidedea wa mashindano hayo kwa Mwaka 2010.
Peter Msechu ameshika nafasi ya Pili na kuipeperusha vyema bendera yetu ya Tanzania katika mashindano hayo. Ametuwakilisha na kutufikisha mahali ambapo hatujawahi kupafikia tokea mashindano hayo yameanzishwa ambapo kwa mara ya kwanza tuliwakilishwa na Mwanamuziki Nakaaya.
Hongera sana Msechu kwa mafanikio hayo. Karibu tena nyumbani uendeleze kipaji chako kwa yale yote uliyayopata ukiwa katika mashindano hayo. Ni imani yangu kuwa Wadau wa Muziki wa Afrika Mashariki wanasubiri ujio wako mpya baada ya kumalizika kwa mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment