Friday, February 26, 2010

WATANZANIA TUNAIPENDA NCHI YETU KWELI JAMANI
Kuna wakati fulani Tanzania tulisikia habari ya kusisimua juu ya mwenendo wa Watanzania kuipenda sana Nchi yao. Hii ni kwa mujibu wa maoni ya utafiti uliofanywa na taasisi ya kimataifa ya utafiti ya Afro Barometer yenye makao makuu nchini Ghana na kuongozwa na Amanda Lea Robinson wa Chuo Kikuu cha Stanford, Marekani.

Nchi ya Tanzania imeweka rekodi ya aina yake barani Afrika kwa kuibuka nchi pekee yenye Wananchi wenye mapenzi makubwa kwa taifa lao kuliko jambo au mfumo wowote wa kitamaduni, kiuchumi au kijamii unaowagawa katika makundi mbalimbali na matabaka.

Na kwa mantiki hiyo kuna yale mapenzi ambayo wakati mwingine mpendaji anaonekana kama "mwehu" kwa wale wasioelewa kuwa mwenzao kapendezwa na nini mpaka kufikia hatua hiyo ya "uwehu."


Mapenzi ya nchi huwa yanaonyeshwa na wazalendo wa nchi kwa namna mbalimbali. Mfano kuna wale ambao Timu yao ya Taifa inapocheza tu utawaona wamejipaka rangi za Taifa usoni,wamevaa fulana za Timu yao,wanapita mitaani wanaimba ili hali tu wenzao wanaoiwakilisha nchi waone kuwa kuna kundi kubwa la wazalendo lipo nyuma yao kuwaunga mkono wawakilishi wao.
Ebu ona mtiririko ufuatao katika Picha.

TAIFA STARS UWANJANI INAPIGA DUA


KOCHA MKUU NA BENCHI LAKE WANAOMBA DUA PIA



Na kama nilivyolueleza hapo awali kuwa uvaaji wa sare zenye kuiwakilisha nchi hauishii kwa Wachezaji, Kocha Mkuu na benchi la ufundi kama tulivyoona katika Picha zilizopita. Uvaaji wa naman hiyo pia hufanywa na Washabiki....hiyo yote ni katika kuonyesha uzalendo kwa Timu yao ikizingatiwa ya kuwa Timu hiyo inaliwakilisha Taifa.

Uvaaji wa Nguo zenye Rangi ya Taifa uwa unaambatana na Ushangiliaji wa nguvu uwanjani. Lengo hapa likiwa ni kuwapanguvu zaidi Wachezaji wacheze kwa bidii kuwafurahisha washabiki huku wakati huo huo wakisaka ushindi kwa ajili ya kulitea sifa Taifa lao.

Na ikumbukwe kuwa Ushabiki haujalishi Timu imeshinda ama imefungwa. Ni kushangalia kwa kwenda mbele tu bila kuchoka. Tena ushangiliaji huwa unanoga zaidi unapowaona Viongozi wakubwa wa Serikali wamejumuika uwanjani wakishangilia kama walivyo washabiki wengine.

USHABIKI WA VIONGOZI UNAONGEZA MORALI ZAIDI


"SAFI VIJANA KAZENI BUTI ZAIDI"


Unajua kila Mtu akishiriki kwa nafasi yake kuiunga Mkono Timu ya Taifa, mwisho wa siku Vijana wanacheza kwa bidii kwa nia ya kupata ushindi. Ushindi ukipatikana sasa...........Ni shangwe ya aina yake bila kujali huyu ni nani wala yule ni nani. Ebu ona hapa......

WASHABIKI WAKIWA WAMEPANDWA NA MZUKA WA USHINDI



Jamani hamna raha kama ya ushindi. Ushindi hauji hivi hivi. Licha ya maandilizi ya kutosha ya Timu lakini Washabiki wana nafasi kubwa sana ya kufanya Timu icheze kwa kujituma. Siku zote tuonyeshe uzalendo ama mapenzi mema kwa Timu yetu ya Taifa,tujitokeze kwa wingi kila inapocheza, tuishangilie bila kuchoka na tukubali matokeo.

Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeshiriki kikamilifu kwa nafasi yetu kuonyesha mapenzi kwa Nchi yetu kupitia anga hizo za Michezo kwani kama nilivyosema hapo awali ni kuwa Mapenzi ya nchi huwa yanaonyeshwa na wazalendo wa nchi kwa namna mbalimbali. Mfano kuna wale ambao Timu yao ya Taifa inapocheza tu utawaona wamejipaka rangi za Taifa usoni,wamevaa fulana za Timu yao,wanapita mitaani wanaimba ili hali tu wenzao wanaoiwakilisha nchi waone kuwa kuna kundi kubwa la wazalendo lipo nyuma yao kuwaunga mkono wawakilishi wao.

NAIPENDA SANA TIMU YANGU YA TAIFA. NAIPENDA SANA NCHI YANGU. MUNGI IBARIKI TAIFA STARS. MUNGU IBARIKI TANZANIA.

No comments:

Post a Comment