Thursday, February 25, 2010

MAJANGA KATIKA MUONEKANO

MJENGO NDANI YA HAITI

Hakuna Jamii hisiyokumbwa na majanga katika Sayari hii ya Tatu maarufu kama Dunia. Na inaeleweka wazi kuwa majanga hayo huleta hofu miongoni mwa wakazi wa eneo husika na hata kwa wale wanaoishi karibu na husika. Wakati mwingine hofu hiyo huwakumba hata wakazi wa mbali....na hiyo inatokana na ile hali ya uhusiano uliopo baina ya pande zote mbili.

Yanapotokea majanga kama hayo sasa (kama ulivyoona katika Picha za hapo juu), vyombo vya habari huwa vinatumia nafasi zao za kuhabarisha Wananchi. Habari hizo huwa zinatolewa kwa njia ya Maandishi lakini pia kuna njia ya Picha. Kwenye Picha kuna ule usemi usemao kuwa, "Picha inazungumza Maneno mengi zaidi ya Maandishi."

Na katika usemi huo, tunaambiwa kuwa ukubwa wa matukio ya majanga mbalimbali duniani huwa yanaelezewa katika Picha kwa kutumia Wanawake na Watoto. Na hata ukweli wa hayo yanayosemwa juu ya hizo Picha tunaweza yaona kwa mfano wa hivi karibuni katika tetemeko la huko Haiti......hebu Picha zifuatazo.




Na ukijaribu kufuatilia matukio ya majanga mengi utaona huo ushahidi wa matumizi ya Picha zaidi za Wanawake na Watoto katika kuelezea ukubwa wa tatizo. Na wakati mwingine pia Wazee wanatumika katika Picha za majanga kama hayo.

Wanawake na Watoto wanatumiaka zaidi kwa kuwa muenekano wao huwa unavuta umakini kwa watu wengine kutaka kujua hasa ni nini kimewasibu wahusika hao. Kama unavyojua, Wanawake na Watoto huwa wanatia huruma sana. Ukiwaona wametumika katika tukio fulani ni lazima utajikuta unapatwa na huruma juu yao.....na mwisho wa siku unashawishika kuwasaidia.

Ila kwa huo mfano wa Haiti,Picha ambayo imefunika kuliko zote na imevuta hisia za watu wengi duniani ni hii utakayoiona punde ambapo mtoto alidumu chini ya jengo kwa siku kadhaa, anafikiwa na kikosi cha uokoaji na anapotolewa tu, anashangilia kwa mikono yote miwili kujiona kwa mara nyingine tena anarudi kwenye mwanga akitokea kwenye giza la chini ya Vifusi vya majengo.

Kwa matumizi ya Picha kama hizo, mwisho wa siku ujumbe unakuwa umefika juu ya janga husika.

No comments:

Post a Comment